Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

MCHANGA NA VIBUYU VILIVYOTUMIKA KUCHANGANYA MCHANGA WA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Imewekwa: 30 Apr, 2026
MCHANGA NA VIBUYU VILIVYOTUMIKA KUCHANGANYA MCHANGA WA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Katika tukio la kihistoria la tarehe 26 Aprili 1964, mchanga kutoka Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa kama ishara ya kuungana kwa nchi hizo mbili na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Tukio hilo lilifanywa na viongozi Tanganyika na Zanzibar, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Vifaa na mchanga vilivyotumika ni:

  • Vibuyu: Udongo kutoka pande zote mbili uliwekwa kwenye vibuyu viwili tofauti kabla ya kuchanganywa.
  • Mchanga (Udongo):
    • Mchanga wa Zanzibar ulichotwa kutoka eneo la Kizimbani, Unguja.
    • Mchanga wa Tanganyika ulichotwa kutoka maeneo ya Dar es Salaam.
  • Chungu: Mwalimu Julius K. Nyerere alichanganya mchanga huo kwa kuumimina ndani ya chungu kimoja katika Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru), Dar es Salaam.

Hadi leo, vibuyu halisi vilivyotumika na mchanga wake vimehifadhiwa na vinaweza kuonekana katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta, Dar es Salaam.