Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Napata faida gani napotembelea Makumbusho ya Taifa?
Kupata uwelewa mpana kuhusu Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla pia Burudani na Kuongeza marafiki wa kimaendeleo.
Makumbusho iko wapi?
Makumbusho ya Taifa Tanzania ni Taasisi ya serikali iliyoko chini ya Wizara ya Maliasili na utalii iliyoanzishwa chini ya sheria ya ya Bunge No.7 ya Makumbusho Ya Taifa Tanzania ya mwaka 1980. Makumbusho ya Taifa ni Taasisi iliyopewa mamlaka ya kukusanya, kuhifadhi, kusimamia, kufanya Tafiti ya urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania kwa kipindi kilichopita na sasa kwa faida ya wanadamu wote. Makumbusho ya Taifa inamatawi saba, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam, Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam, Azimio la Arusha, Arusha, Elimu Viumbe, Arusha, Makumbusho ya Majimaji, Songea, Makumbusho ya Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, Songea, Makumbusho ya Mwalimu Nyerere, Butihama - Mara.
Ukumbi wa Maonesho ya Jukwaani unachukuwa watu wangapi?
Una viti 470 tu.
Nimuda gani Makumbusho inakuwa wazi?
Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.
Makumbusho inahifadhi vitu vya kale tu?
Makumbusho inahusika na uhifadhi wa urithi wa utamaduni na asili unaohamishika. Urithi huu waweza kuwa wa kale na wa sasa.
What is museum
A museum is an institution that cares for (conserves) a collection of artifacts and other objects of artistic, cultural, historical, or scientific importance
ninyi ni nani
MAKUMBUSHO YA TAIFA TANZANIA
Ni nani Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa of Tanzania?
Prof Audax Mabula