MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA YAPOKEA WATALII WA MELI YA KIFAHARI SEVEN SEAS VOYAGER
Makumbusho ya Taifa la Tanzania yanayo furaha kuwakaribisha wageni zaidi ya 500 waliowasili nchini kupitia meli ya kifahari Seven Seas Voyager tarehe 18–19 Februari 2026.Ujio wa watalii hao ni fursa adhimu kwa taifa letu kuendelea kutangaza na kuonesha utajiri wa urithi wa kihistoria, kitamaduni na malikale tulionao.
Kupitia ziara zao katika vituo vya Makumbusho, wageni wanapata nafasi ya kujifunza historia ya Tanzania, kushuhudia mabaki ya kale, pamoja na kufahamu mila na desturi zinazolitambulisha taifa letu kimataifa.
Makumbusho ya Taifa la Tanzania yataendelea kushirikiana na wadau wa utalii kuhakikisha kila mgeni anapata uzoefu wa kipekee, elimu sahihi ya urithi wetu, na kumbukumbu zisizosahaulika.
#DestinationNationalmuseum
#TanzaniaBeyondSafaris
#TwenzetuMakumbusho

