Paleontolojia

PALEONTOLOJIA.

Paleontolojia ni sayansi inayohusu maisha ya kale hasa kwa kujifunza mabaki ya wanyama na mimea. Mabaki haya huashiria maisha ya awali na hutumiwa kama dirisha la kijifunza mabadiliko mbali mbali wanyama au mamalia, binadamu na mazingira ya kale kwa ujumla.

Kuhusu Mikusanyo.

Mikusanyo ya Paleontolojia ndiyo iliyo kuu na nyingi ikiwemo baadhi ya masalia ya Zamadamu bora duniani ikiwemo fuvu maarufu la Zinjanthropus ambayo huvutia watafiti wengi kutoka ndani na nje ya nchi. Mikusanyo ya Paleontolojia katika Makumbusho ilianza kukusanywa toka kipindi cha ukoloni mwaka 1930 na inaendelea hadi leo. Baadhi ya mikusanyo ni mikubwa sana na huwakilisha wanyama wa zama za kale kama vile tembo na mingine huwakilisha mamalia wadogo kama panya. Mikusanyo hii hupatikana kwa njia ya utafiti na baada ya utafiti kukamilika huletwa Makumbusho kwa ajili ya kuhifadhiwa na kuwekwa kwenye maonesho kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii.

Tafiti mbalimbali kusuhu mikusanyo hii husaidia kuelewa maisha ya kale ya wanyama , binadamu, mimea na hata mazingira yao. Pia tafiti hizi husaidia namna bora ya kuhifadhi mazingira kama njia pekee ya kulinda urithi wetu wa asili.

Lengo letu ni kuongeza uelewa wa umma kuhusu kisayansi, mazingira na historia ya masalia ya kale “Paleontology” kwa njia ya tafiti mbalimbali na hasa masalia ya kale ya wanyama, zamadmu “hominin” na mimea. Mbali na kufanya utafiti wa kisayansi, Makumbusho hutoa elimu hii kwa umma kwa njia ya mafunzo, vyombo vya habari, machapisho, maonyesho, ziara mbalimbali na mazungumzo au majadiliano kwa wanafunzi.