Elimu Viumbe

HISTORIA YA MAKUMBUSHO

Makumbusho ya Historia asilia Arusha ilifunguliwa mwaka 1987, na ni Mkaumbusho pekee nchini ya Historia asilia. Makumbusho hii ipo katika mji mkuu wa utalii Arusha ndani ya Afrika Mashariki. Makumbusho hii imejikita katika kutunza na kuhifadhi mikusanyo ya sampuli mbalimbali za Historia asilia, ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa kina wa masalia ya mifupa ya wanyama wenye uti wa mgongo pamoja na Historia ya mji wa Arusha - Boma.


CHIMBUKO

Makumbusho ya Historia asilia ipo katika Boma la zamani la kijeshi na ulinzi wa ukoloni wa wajerumani. Mtindo wa awali uliboreshwa na wakazi wa mji wa Boma baada ya kipindi cha utawala wa Ujerumani. Kwa hiyo, manamo mwaka 1996 mkoa wa Arusha na mji mkuu wa Brussels (Belgium) walianzisha mradi wa maendeleo kati ya mwaka 1996 hadi 1998 ili kusaidia Boma la wajerumani na Makumbusho ya Historia asilia.SABABU ZA KUANZISHWA

Uamuzi wa kutumia Boma la Wajerumani kwa madhumuni ya Makumbusho alichukuliwa mwaka 1984 na serikali, kupitia Makumbusho ya Taifa ya Tanzania. Hii ilihalalishwa kwa nafasi ya kipekee kwa Tanzania kuchukua nafasi katika historia ya mwanadamu na utajiri wa urithi wake wa asili. Makumbusho ilikuwa sharti kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa mikusanyo ya kisayansi (palaeontolojia, zoolojia, mimea na jeolojia) pamoja na kuonyesha kwa madhumuni ya elimu na starehe.

Mkakati wa muda mrefu wa Makumbusho ni kutoa vitendea kazi kwa ajili ya mikusanyo ya sayansi asilia, mafunzo ya wahifadhi na “Taxidermists”kwa ajili ya kuonyesha ya urithi wa asili wa nchi. Tanzania kuwa tajiri na maarufu kwa masalia ya “fauna” ikiwa ni pamoja na masalia ya “hominids” katika tabaka la kijiolojia la Olduvai Gorge, Peninj na Laetoli na kuipa kipaumbele kuwa mlinzi kwa nchi kutoa mchango wa jamii ya kisayansi na utunzaji wa hazina ya Taifa.


KUHUSU MIKUSANYO


KUMBI ZA MAONYESHO


PROGRAMU ZA KAWAIDA / MATUKIO NA HUDUMA

Wageni wa umri wote na mataifa wanakaribishwa kuona hazina na kufurahia maonyesho yetu na vitu ambavyo huelimisha kuhusu historia asilia ya Tanzania, iliyoundwa kwa ajili ya tafiti zote, elimu na burudani. Makumbusho ina timu nzuri ya watendaji wenye elimu ya Makumbusho na wahifadhi kwa ajili ya kuongoza matembezi kuzunguka kumbi za maonyesho, viwanja vya makumbusho na jengo kihistoria "Boma". Timu pia husaidia wanafunzi katika tafiti wanazofanya.

Kituo cha huduma ya mtandao inatoa rejea za ziada kwa wanafunzi na umma kwa ujumla juu ya masuala ya mbalimbali binafsi kuhusu mada za tafiti zao.

Makumbusho imejitolea kuleta zana za kisayansi na taarifa zake kwa watazamaji nchini kote kupitia njia ya programu za kufikika, video, warsha na mikutano na shughuli za mradi kwa makundi ya shule na ya umma.

Maonyesho ya kudumu ya picha za Wanyamapori wazuri na wakubwa duniani ni kazi mashuhuri ya mpiga picha wa wanyamapori Dick Persson.


MAWASILIANO

S.L.P 2160

Boma Road, Arusha

Simu no. +255 27 254 5540

Barua pepe: nnhm@habari.co.tz

ENEO:

Makumbusho ya Historia ya asili ya Taifa iko mwisho wa Boma road jirani na “Arusha International Conference Centre (AICC)”, Halmashauri ya Jiji la Arusha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

MUDA WA KAZI:

VIINGILIO: