WANAWAKE WATAKIWA KUPIGANIA HAKI ZAO

Imewekwa: 10th March, 2020

Wanawake wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania waliungana na wanawake wengine duniani kusherehekea siku ya Wanawake Duniani katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam na Arusha mjini.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ambae aliekuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo, aliyapokea maandamano ya akina mama hao na pia aliwapongeza kwa juhudi za kujiletea maendeleao yao na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Mhe. Makonda aliwataka wanawake kuendelea kupigania haki zao katika ngazi zote na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inawaunga mkono.

Endeleeni kupigania haki zenu ikiwa ni pamoja na kushika nafasi za uongozi maeneo mbalimbali na Serikali iko pamoja nanyi” alisema Mhe. Makonda.

Alisema kuwa Serikali inathamini mchango wa wanawake katika kutunza familiya na malezi mema kwa watoto wa kitanzania.

Awali wanawake waliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa msaada wa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu ambayo imewasaidia katika kujiletea maendeleo na kujipatia kipato cha kutunza familiya zao.

Waliomba Serikali iwasaidie katika kupata masoko ya biashara zao kwa sababu wamekuwa wakizalisha kwa wingi lakini soko la bidhaa hizo imekuwa changamoto.

Kwa upande mwingine Wanawake wa Makumbusho ya Taifa walimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho, Dkt Noel Lwoga kwa kuona umuhimu wa ofisi yake kuwawezesha wanawake hao ili waweze kushiriki na wanawake wenzao Duniani.

Ushiriki wetu leo umetufanya tujioni kweli tunathaminiwa na uongozi wetu wa Makumbusho, hii inafaida kubwa sana kwa Taasisi yatu maana leo tumeisogeza Makumbusho ya Taifa kwa wanawake wenzetu, Mungu awabariki Viongozi wote wa juu wa Shirika letu la Makumbusho” Alisema mmoja wa mama walioshiriki.