emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

UBALOZI WA FINLAND WAVUTIWA NA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO NCHINI.


Ubalozi wa Finland nchini Tanzania leo wamekitumia Kijiji cha Makumbusho katika kusherehekea siku yao ya Burudani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Novemba. Wakiongozwa na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini Mhe. Riita Swan ndani ya Kijiji cha Makumbusho maafisa na wafanyakazi mbali mbali wa Ubalozi huowalipata kutembelea nyumba mbalimbali za asili, kujifunza kupiga na kucheza muziki na ngoma za asili ya makabila ya kitanzania. Vile vile waliweza kupata chakula cha asili katika mgahawa mpya wa Brake Point.


Wageni hao walipokelewa Kijiji hapo na Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Dkt Gwakisa Kamatula.

Akizungumzia sababu za kukitumia Kijiji cha Makumbusho kwa maadhimisho hayo Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riita Swan amesema kuwa wamevutiwa na urithi wa kiutamaduni uliopo ndani ya Makumbusho hiyo hivyo wameona ni vyema wauenzi utamaduni wa Mtanzania na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kila mwaka.

Akipongeza hatua hiyo iliyochukukiwa na Ubalozi wa Finland hapa nchini Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Tanzania Dkt. Noel Lwoga ametoa wito kwa Taasisi nyingine nchini na wananchi kwa ujumla kufanya shughuli zao za mapumziko na burudani Makumbusho ya Taifa na maeneo ya Malikale kwani, pamoja na burudani, watajifunza utamaduni na historia ya nchi.