Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA YAPOKEA SEHEMU YA KWANZA YA VIFAA VYA AWALI VYA UHIFADHI MIKUSANYO KUTOKA MAKUMBUSHO YA OMAN

Imewekwa: 06 Feb, 2024
MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA YAPOKEA SEHEMU YA KWANZA YA VIFAA VYA AWALI VYA UHIFADHI MIKUSANYO KUTOKA MAKUMBUSHO YA OMAN

Waziri wa Utalii na Maliasili Mhe. Angellah Kairuki leo tarehe 6 Februari 2024 ameshuhudia makabidhiano ya sehemu ya kwanza ya vifaa vya uhifadhi kutoka katika Makumbusho ya Taifa ya Sultani wa Oman jijini Dar es Salaam.



Makabidhiano hayo yaliyofanywa na Mtendaji Mkuu wa Makumbuaho ya Taifa ya Sultan wa Oman, Mhe. Jamaal Al Moosawi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga.

Mhe. Kairuki amepongeza hatua hiyo na kusema ni mwanzo mzuri wa utekelezaji kati ya yale maeneo matano yaliyopangwa kufanyiwa kazi ikiwemo masuala ya Utafiti, Uhifadhi, Kujengeana uwezo na Ujenzi wa jengo la utamaduni wa Kiswahili na Oman.



Naye Dkt. Noel Lwoga ameshukuru mwanzo wa utekelezaji mzuri wa mambo waliyojadiliana toka kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano kati ya Makumbusho ya Tanzania na Oman Juni mwaka 2022.

Wataalam kutoka Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Makumbusho ya Taifa ya Sultan wa Oman wamekutana ili kuainisha maeneo ya kuweka mradi wa jengo la kiutamaduni la Kiswahili na Oman na eneo ambalo litaboresha Onesho la Historia nchini, kupitia mikusanyo yote ambayo ina viashiria vya mashirikiano baina ya Oman na Tanzania.

Tanzania na Oman ilisaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) tarehe 13 Juni 2022.