​MAKUMBUSHO YA TAIFA KUIMARISHA MFUMO WA MAWASILIANO WA KIDIJITALI

Imewekwa: 11th May, 2020

MAKUMBUSHO YA TAIFA KUIMARISHA MFUMO WA MAWASILIANO WA KIDIJITALI

Makumbusho ya Taifa nchini imeweka mikakati ya kuimarisha mifumo ya kimawasiliano kidijiitali ili kuendana na kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

Akizungumza katika kikao maalumu cha kupitia hatua za Maboresho ya Mifumo hiyo kilicho udhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya uongozi wa Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ni wakati sasa wa kuhakikisha Makumbusho inatumia njia rafiki na zenye kuvutia katika kuifanya Taasisi iwasiliane na umma.

Mifumo hii ikiboreshwa itasaidia sana watu mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kupata taarifa za huduma zetu kwa haraka zaidi, kupokea taarifa kutoka kwenye vyanzo mbali mbali, pia licha Taasisi yetu kuonekana ya kisasa zaidi, mapato yetu yataongezeka” Aliongea Dkt Lwoga

Akielezea hatua mbali mbali zilizo fikiwa katika Maboresho hayo, Mkuu wa kitengo cha TEHAMA Bw Lusekelo Kaisi alisema kuwa muda si mrefu Tovuti ya Taasisi itakuwa na mwonekano mpya na yenye taarifa nyingi na zenye kuvutia.

Kitengo cha TEHAMA kimejizatiti kuhakikisha vikao vinaendeshwa kidijitali kama njia ya mapambano ya homa kali ya Mapafu inayo sababishwa na Virusi vya KORONA na pia kuipunguzia Taasisi gharama”. Alisema Bw Kaisi.

Kikao hicho kilicho fanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kilihusu maboresho ya Tovuti ya Shirika, uwendeshaji wa vikao vya kiofisi, ukusanyaji wa taarifa kutoka katika vituo vya Makumbusho nchini na kutoka kwa vyanzo mbalimbali nje ya Makumbusho za Taifa.