emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

MAKUMBUSHO INAYOTEMBEA YANOGESHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.


MAKUMBUSHO INAYOTEMBEA YANOGESHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Na Joyce Mkinga

Makumbusho ya Taifa nchini imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kwa kuelimisha jaamii juu ya Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na Malikale kupitia Gari Maalumu (Makumbusho inayotembea).

Katika Maadhimisho hayo ambayo yalijumuisha maandamano ya wanawake kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na mashirika binafsi pamoja na wajasiriamali wa Jijini Dar es Salaam, wengi wao walifika na kushiriki program za kielimu ikiwemo kusaga ulezi kwa kutumia mawe na kusuka ukiri.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, ameipongeza Makumbusho ya Taifa Kwa ubunifu huyo kubwa wa kuhakikisha watanzania wananufaika na elimu ya kimakumbusho popote walipo na kutoa wito kwa wananchi kuunga Mkono juhudi hizo kwa kujitokeza kuitembelea Makumbusho hiyo itakapokuwa kwenye maeneo yao.

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa, Bi Anamery Bagenyi ameeleza kuwa gari hilo limenunuliwa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa lengo la kutangaza utalii wa Makumbusho na Malikale ili watu wengi zaidi waweze kujua.“Kuna watu wako mbali na Makumbusho na vituo vya Malikale hivyo gari hii itasaidia katika kuifikia jamii” alisema Bi Bagenyi.

Gari hilo ambalo limenunuliwa kwa fedha za Mpango wa Ustawi wa Jamii na Kuthibiti Maambukizi ya UVIKO 19 ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Taasisi ya Makumbusho ya Taifa wa kuwafikia wananchi wengi zaidi na kushirikisha jamii katika masuala ya Makumbusho na Malikale.

Aidha, Mpango wa Masoko wa Taasisi hiyo umeainisha njia mbalimbali za kutangaza makumbuhso na Malikale nchini ikiwemo Maonesho, matangazo na programu za kielimu ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia program ya Royal Tour ambayo inalenga katika kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.