Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

MAAFISA WANAMICHEZO ZAIDI YA MIA TATU KUTEMBELEA MAKUMBUSHO

Imewekwa: 31 Jan, 2024
MAAFISA WANAMICHEZO ZAIDI YA MIA TATU KUTEMBELEA MAKUMBUSHO

 

Siku ya tarehe 30/1/2024 baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Itifaki ya Baraza la michezo la Majeshi Duniani (CISM) wakiwa wameambatana na Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wametembelea kituo Cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam  kwaajili ya maandalizi ya ugeni wa Wanajeshi Wanamichezo zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali duniani wanaotarajiwa kutembelea kwenye vituo vya Makumbusho na maeneo mengine ya Utalii baadae mwezi Mei mwaka huu 2024