BALOZI WA USWISI AIPONGEZA MAKUMBUSHO YA TAIFA

Imewekwa: 31st May, 2019

Na Sixmund J. Begashe

Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Florence Mattli ameishauri makumbusho ya Taifa kuongeza ubunifu katika kutoa elimu juu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira na kuzipa thamani takataka.

Balozi ameyasema haya jana alipotembelea Makumbusho ya Taifa na kufanya mazungumzo na uwongozi wa Makumbusho hiyo pamoja na kutembelea chumba maumhususi kinahifadhi vioneshwa vya dhamani likiwemo fuvu la zinjanthropus.

Amesema Makumbusho ya Taifa inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuisaidia jamii kupambana na changamoto ya ukusanyaji takataka na kuzipa thamani takataka kwa kutengeneza bidhaa zinazotokana na takataka hizo.

“Nashauri muweke maonesho yatakayo onesha namna wabunifu walivyozifanya takataka kuwa bidhaa inayo vutia, hiyo itawavutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi ” alisema Mhe. Mattli.

Balozi Mattli pia ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa jitihada kubwa za kuielimisha jamii juu ya changamoto mbali mbali kupitia Maonesho na program za mara kwa mara za ndani na nje ya Makumbusho kama ile ya Museum Art Explosion.

Licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa, Balozi Mattli amehahidi kuwa Ubalozi wa Uswisi utaendekea kushirikina na Makumbusho ya Taifa kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika kuwapatia wananchi wake maendeleo, kwa kuelimisha jamii namna ya kupambana na changamoto mbali mbali zinazo wakabili.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabulla alimshukuru Balozi wa Uswisi kwa ufadhili wa miradi mitatu Makumbusho ya Taifa ambayo ni Mapambano Dhidi ya Rushwa 2017, Mapambano Dhidi Mimba za Utotoni 2018 na Mapambano Dhidi ya Uharibifu wa Mazingira kwa mwaka huu (2019).

Prof Audax Mabula, amemhakikishia Balozi huyo kuwa Makumbusho ya Taifa itaendelea kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi katika mambo yote yenye maslai mapana ya nchini na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Kwa niaba ya Makumbusho ya Tafa, nakushukuru sana kwa kututembela, kuendelea kuunga mkono jitihada zetu hasa kupitia programu ya Museum Art Explosion, pia tunakushukuru sana kwa ushauri ulio tupatia juu ya kuwa na maonesho elimishi juu ya utunzaji wa mazingira, nakuahidi kuwa tutafanyia kazi ushauri wako na tutaendelea kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi” Alisema Prof Mabula.

Mhe Balozi Mattli aliyeongozana na Bw. Momar Seck Msanii Mkongwe wa Sanaa za ufundi nchini Uswisi mwenye asili ya Senegali, walipata nafasi ya kutembelea chumba Mahususi ili kujionea Kinyago cha kimakonde kilichoibiwa na kupelekwa nchini Uswisi na kisha Serikali ya Tanzania kukirudisha nchini pamoja na kujionea fuvu la anayesadikiwa kuwa ni binadamu wa kale aliyeishi zaidi ( Zinjanthropus ) ya miaka milioni 1.7 iliyopita lililo hifadhiwa katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.

Mwisho