emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

BALOZI. DKT, PINDI CHANA AZINDUA BODI YA MAKUMBUSHO YA TAIFA


Na Mwandishi Wetu,

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt Pindi Chana amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa na kuwataka kulisimamia shirika ili liweze kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 22 Oktoba 22, Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kuhakikisha kwamba wamashirikiana kikamilifu na Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa ili kufikia lengo la Serikali la kuongeza watalii kufikia watalii milioni tano na mapato ya billion sita ifikapo mwaka 2025.

“Bodi kwa kushirikiana na menejimenti, mnatakiwa kufanyakazi kwa kutazama lengo hili la kuongeza idadi ya watalii na mapato, amesema Mhe.Waziri.

Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana ameipongeza Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa pamoja na watumishi wake wote wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Noel Biseko Lwoga, kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kipindi chote ambacho Bodi haikuwepo.

Amesema kumekuwa na maboresho makubwa katika masuala mbalimbali ikiwemo uhifadhi, tafiti, elimu kwa jamii, uboreshaji wa baadhi ya miundombinu ya uhifadhi, uhifadhi wa malikale na kutangaza urithi wa Taifa kupitia matukio na matamasha mbalimbali, na hata kuongezeka kwa wageni wa ndani kutoka elfu sabini (70,000) iliyozoeleka huko nyuma hadi wageni wa ndani zaidi ya laki saba (700,000) kwa mwaka 2021/22.

“Ni matumani yetu sisi kama Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba Bodi hii itashirikiana vizuri na Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kuendeleza kazi hizi nzuri kwa kasi zaidi, na kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya Makumbusho na Malikale kwa ujumla” alisema Mhe. Waziri.

Amesema kuwa Makumbusho ya Taifa la Tanzania ilianzishwa kwa sheria Namba 7 ya mwaka 1980 ambayo inafanyiwa marekebisho, na sasa zimeandaliwa Kanuni za utekelezaji wa Sheria hiyo. Nichukue fursa hii kuwakumbusha kutekeleza majukumu yenu kulingana na sheria hiyo, na kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya Serikali.

“Hivyo Bodi hii inawajibu wa kusimamia Shirika la Makumbusho ya Taifa kuhakikisha kwamba utamaduni na urithi wa Taifa unahifadhiwa na kuendelezwa ipasavyo “ Alisema Mhe Waziri.

Balozi. Dkt. Pindi chana alimpongeza Mwenyekiti wa Bodi pamoja na wajumbe kwa kuteuliwa pamoja na menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kwa kuwa timu moja inayotafuta ushindi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Oswald Masebo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuwateua wajumbe wa Bodi hiyo na kuhaidi kuwa watashirikiana vizuri na menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kuleta maendeleo katika Taasisi.

“Mhe. Waziri naomba nikuhakikishie utayari wetu wa kushirikiana na menejimenti ili kuleta maendeleo chanya katia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa na Malikale,” Alisema Mwenyekiti wa Bodi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa, Dkt. Oswald Masebo vitendeakazi mara baada uzinduzi wa Bodi hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Pindi Chana katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa

Waziri wa Maliasili ba Utalii, Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakiwa wameshikana mikono kama ishara ya umoja