Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Mapango ya mlima Chandamali

Imewekwa: 11 Jan, 2024
Mapango ya mlima Chandamali

Mapango ya mlima Chandamali ni moja ya sehemu iliyotumiwa kimkakati na kiongozi wa vita vya Majimaji Nduna Songea Mbano eneo hilo linapatikana nje kidogo kutoka katika viwanja vya Makumbusho ya Majimaji eneo la mlima chandamali ndio eneo yanapopatikana mapango ambayo yalitumika kipindi cha vita ya Majimaji kama sehemu ya maficho kwa chifu Songea Mbano pia juu ya mapango hayo ndipo alipokuwa anatumia kukaa na kuangalia maadui zake wakiwa katika umbali mrefu, katika mapango ya mlima chandamali shughuli mbalimbali za mila na desturi zilikuwa zikifanyika na bado zinaendelea kufanyika mpaka sasa na ndio eneo pekee lenye sifa ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wa kimila tangu kipindi cha vita vya Majimaji mpaka sasa, katika eneo hili pia ni moja ya sehemu ambazo mjerumani alishindwa kuingia na kukamata wapiganaji wa vita vya Majimaji.

Karibu Kituo cha Makumbusho ya Vita ya Majimaji - Songea kupata kujua namna Chifu Songea Mbano alivyopambana na Utawala wa Kikolono wa Wajerumani kipindi cha vita ya majimaji,

Mawasiliano

Majimaji Memorial Museum

P.O BOX 1249 Songea,

 Tanzania

Mobile: +255 786 472700

Email: majimaji@nmt.go.tz