MASIMULIZI

MASIMULIZI

Makumbusho ya Taifa kupitia Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni huandaa program za masimulizi kwa watoto ili kutoa nafasi kwa watu wazima kurithisha uridhi wa utamaduni wa masimulizi kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Kupitia program ya masimulizi watoto kutoka sehemu mbali mbali ujifunza namna ya kufanya masimulizi, umuhimu wa masimulizi kwa jamii hususani kwa watoto wa kitanzania pia wazee kutoka sehemu mbali mbali usimulia watoto simulizi zenye lengo la kurithisha falsafa za Mshikamano, Upendo, Umoja na namna ya kupambana na maadui wa kila siku wa maisha ya binadamu.