Historia ya Taasisi

UTANGULIZI

Makumbusho ya Taifa Tanzania ni Taasisi ya serikali iliyoko chini ya Wizara ya Maliasili na utalii iliyoanzishwa chini ya sheria ya ya Bunge No.7 ya Makumbusho Ya Taifa Tanzania ya mwaka 1980. Makumbusho ya Taifa ni Taasisi iliyopewa mamlaka ya kukusanya, kuhifadhi, kusimamia, kufanya Tafiti ya urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania kwa kipindi kilichopita na sasa kwa faida ya wanadamu wote. Ukusanyaji wa urithi na maelezo yake zimewekwa kwenye masanduku ya maonyesho kwa Madhumuni ya kuendeleza maarifa, kuthamini na matumizi endelevu kwa watu wote, kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kupitia maonyesho yake na mipango ya elimu , Makumbusho imekuwa chombo cha maendeleo kwa kulenga vitendo na matukio ili kuhimiza maendeleo katika jamii. Aidha, Makumbusho ni chombo kinachotumika kukuza amani na kukuza maadili ya demokrasia na uwazi katika utawala bora kwa jamii, na wakati huohuo kukuza Taifa na umoja ulimwenguni na uhifadhi wa utofauti za tamaduni.

Makumbusho ya Taifa Tanzania inaunganisha vituo sita ambavyo ni:

  1. Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
  2. Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam
  3. Makumbusho ya Elimu viumbe Arusha
  4. Makumbusho ya Azimio la Arusha
  5. Makumbusho ya Mwalimu Julius K. Nyerere Butiama
  6. Makumbusho ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji Songea.

Kila moja ya makumbusho hiyo ni nyumba ya kipekee, kitajiri na ina vitu vya asili na tamaduni za urithi wa Taifa.