Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

WAZIRI CHANA, DKT. ABBASI WAKUTANA NA MACHIFU, SONGEA

Imewekwa: 23 Sep, 2024
WAZIRI CHANA, DKT. ABBASI WAKUTANA NA MACHIFU, SONGEA

Machifu wa makabila mbalimbali nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuungana na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kuimarisha amani na Utulivu nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 22 Septemba 2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) aliyeambatana na Katibu Mkuu,  Dkt. Hassan Abbasi Mkoani Ruvuma alipokutana na Machifu kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini waliofanya ziara ya kutembelea Makumbusho ya Historia ya Vita vya MajiMaji Mjini Songea kama sehemu ya Maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuitembelea Makumbusho hiyo hapo kesho. 

Mhe. Chana aliwahakikishia Machifu hao kuwa Wizara anayoiongoza itaendelea kushirikiana nao  kikamilifu katika Uhifadhi na kuendeleza urithi wa Kihistoria nchini ili watanzania waweze kunufaika na Mazao hayo ya Utalii wa Historia na Malikale. 

Pamoja na kukutana na Machifu hao, Mhe. Balozi Chana amekagua maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Samia kwenye Makumbusho hiyo iliyohifadhi Historia adhimu na adimu katika ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla dhidi ya Ukoloni Miaka takribani 119 iliyopita.