Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Dkt. ABBASI: RAIS SAMIA ANAIENZI HISTORIA YA VITA MAJIMAJI KWA VITENDO

Imewekwa: 20 Sep, 2024
Dkt. ABBASI: RAIS SAMIA ANAIENZI HISTORIA YA VITA MAJIMAJI KWA VITENDO

Na Mwandishi Wetu, Nandete

Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelezwa kuwa mmajimui wa Kiafrika anayeenzi mchango wa wapigania uhuru kwa vitendo ikiwemo historia ya vita ya Maji Maji iliyoazishwa na wazalendo wa kabila la Wamatumbi na kuenea eneo kubwa la jamii za Kusini kupinga ukoloni wa Kijerumani kati ya mwaka 1905 hadi 1907.

Hayo yamesemwa leo kijijini Nandete Kata ya Kipatimu, Kilwa, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi akifunga Tamasha la kuadhimisha miaka 119 ya Vita ya Majimaji.

“Wazee wetu walioongoza vita ile chini ya Jemedari Mkuu Mzee Kikwako Mbonde na mwanafalsafa wake mkuu na mhamasishaji Mohammed Ali Kinjekitile Ngwale walipandikiza mbegu ya ari ya uhuru na uzalendo ambayo leo Rais wetu Dkt. Samia Suluhu anaienzi kwa kuleta maendeleo,” alisema Dkt. Abbasi na  akiongeza:

“Rais Samia pia anawaenzi wapigania uhuru hawa wa Vita vya MajiMaji kwa vitendo kwani ni mwaka huu; miaka 119 baadaye ambapo Serikali yake imeyatangaza rasmi kupitia GN 163 na 166 maeneo ya Nandete yaliyohusika na vita hiyo kuwa urithi wa Taifa na Kimataifa.”

Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohammed Nyundo, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Mhe. Francis Ndulane, viongozi wa kimila, familia za wapigania uhuru hao na mamia ya wananchi, kwa niaba ya Wizara, Dkt. Abbasi ameahidi kumwomba Mhe. Rais Samia kusaidia katika ujenzi wa Makumbusho Maalum ya Vita hiyo mahali ilipoanzia Julai 15, 1905, ambapo wananchi waling’oa pamba katika shamba la wakoloni wa Kijerumani.

Katika maadhimisho hayo wadau mbalimbali wamechangia vitu mbalimbali katika maandalizi ya Tamasha kubwa zaidi la mwakani ambapo Vita ya Maji Maji itafikisha miaka 120 ikiwa ni pamoja na mchele zaidi ya kilo 1,500 umeahidiwa, mafu