Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

SERIKALI IMEANZA KUANDAA MPANGO WA UREJESHAJI MALIKALE ZILIZOKO UJERUMANI

Imewekwa: 28 Feb, 2024
SERIKALI IMEANZA KUANDAA MPANGO WA UREJESHAJI MALIKALE ZILIZOKO UJERUMANI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa Serilikali imeanza kuandaa mpango wa majadiliano ya namna ya kuzirejesha malikale zilizopo katika Taifa la Ujerumani ambapo baadhi ya malikale hizo ni kutoka katika Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mhe. Kairuki amesema haya katika hotuba ya Kilele cha Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas katika Makumbusho ya MajiMaji, mjini Songea.

Mhe. Kairuki amesema kuwa wakati wa utawala wa Wajerumani katika mkoa wa Ruvuma ziko Malikale nyingi zilizochukuliwa na kupelekwa Taifa la Ujerumani na kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuzirejesha ili Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla inufaike nazo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba  amesema kuwa Tamasha hili hutoa fursa kwa Wananchi kushiriki katika kuhifadhi, kuenzi na kuendeleza uzalendo, amani na mshikamano vitu ambavyo ni urithi kutoka kwa Mashujaa wa vita vya Majimaji lakini pia kuchochea na kuibua vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika Kanda ya kusini.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania,  Bi.Mistica Ngongi amesema vita vya Majimaji inawakumbusha nia thabiti ya Watanzania wa enzi hizo ya kuilinda jamii yao, lakini pia inawakumbusha Watanzania tunu za uzalendo, ari, ujasiri, uthubutu na umoja wao kwa maslahi makubwa ya Taifa la Tanzania.

Naye Chifu wa kabila la Wangoni Inkosi wa Makosi Zulu Gama amesema ni muhimu kuendelea kuwaenzi mashujaa wa vita vya Majimaji kwa kuwaombea kwa kuwa walishiriki kwa uaminifu kurithisha tunu ya amani na uzalendo na maadili mema kwa kizazi kilichopo sasa.

Kilele cha Tamasha la Vita vya Majimaji hufanyika kila ifikapo 27 Februari kila mwaka ambapo lilitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo mashindano ya ngoma za asili kwa halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma, Kongamano la Wadau kuhusu Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na maadhimisho ya Siku ya Wangoni katika kijiji Cha Maposen