Maendeleo ya Makumbusho

UANZISHWAJI WA MAKUMBUSHO

Makumbusho inatoa ushauri jinsi ya kuanzisha makumbusho, na pia hutoa ushauri wa kiufundi kuhusiana na uhifadhi na marejesho ya vifaa ( mikusanyo ) vya urithi., vivutio vya kisayansi ni pamoja na vyote vinavyoshikika na visivyoshikika vya utamaduni au asili vinavyoonekana kuchukuliwa thamani ya kuwa mikusanyo ya kisayansi, kitamaduni, kihistoria , kiteknolojia, kisanii kama vile vitu vya thamani, kwa elimu, rufaa, utambulisho na madhumuni ya burudani ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Na pia Makumbusho inatoa ushauri juu ya jinsi ya kupanga mikusanyo kwa mujibu wa makundi yao kama historia, baiolojia, sanaa, paleontolojia, jiolojia au mila.