Uhifadhi

UTUNZAJI YA MIKUSANYO YA MAKUMBUSHO

Makumbusho hukusanya vitu ya aina mbalimbali ambavyo vinahitaji huduma endelevu ili kuvihifadhi. hatari nyingi hutishia maisha ya mikusanyo ya makumbusho. Ni dhahiri kwamba mikusanyo ya Makumbusho haiishi milele, lakini tahadhari inaiawezesha mikusanyo kuvumilia kwa karne zijayo. Ni wajibu wa makumbusho yoyote ile kuhakikisha kuwa mikusanyo ya makumbusho inapata huduma kupitia njia mbalimbali za matibabu.

Utunzaji wa vitu vya Makumbusho unahusisha hatua kuu nne ambazo ni lazima zifanyike mara kwa mara:


Vitu (mikusanyo) vinayohitaji uangalizi wa hali ya juu:

Makumbusho pia hukusanya mikusanyo ambayo inahitaji uangalizi wa dharura. Mikusanyo hiyo ni ile inayochoka haraka na huitaji huduma mara moja na kwa haraka. Mashambulizi ya wadudu, vyuma kupata kutu au kuharibika kwa rangi ya mafuta. wadudu wanaoota juu ya mikusanyo wanatakiwa kuuawa mara moja kwa sababu vitundu huendelea haraka na inaweza kusababisha maambukizi kuenea kwa vitu vingine.

Inashauriwa mikusanyo / vitu vilivyoharibiwa sana vinatakiwa vikusanywe na kuwekwa nje kuzuia kuambukiza maeneo mengine yenye mikusanyo. Mikusanyo iliyovukizwa na mikavu huifadhiwa kwenye unyevu wa chini ya 55%. Kwa mikusanyo mingine ambayo sio rahisi kuvukizwa inawekwa kwenye ardhi iliyokaushwa na sponji au kitambaa kilichokaushwa.

Umuhimu wa vibandiko vyenye maelezo kwenye mikusanyo:

Mikusanyo ya mimea na wanyama ina thamani kisayansi kama tu itakuwa na taarifa sahihi. Kwa hiyo ni muhimu kwa sampuli (Mikusanyo) zote kuwekwa maelezo kamili kabla ya kuanza kupewa huduma. Maelezo yanatakiwa kuwa ya muda mrefu na kuwa na uwezo wa kuhimili kuzamishwa muda mrefu kwenye vimiminika kama vile maji na vilevi.

Na taarifa muhimu ni pamoja na hizi zifuatazo:

Uhusika wa Sehemu : Hii ni mahali ambapo specimen zilikusanywa.Taarifa husika lazima ziwe sahihi iwezekanavyo ili kwamba watafiti wengine waweze kuwa na uwezo wa kujua sehemu mikusanyo imepatikana. Taarifa hizo ni pamoja na Nchi, Mkoa, Wilaya au Vijiji kama vile mwinuko au mawimbi kwa vielelezo vya kibaiolojia. Taarifa hizo pia ni pamoja na maelezo mafupi ya makazi.

Muda: Ni muhimu kurekodi mwezi, tarehe na mwaka wa mikusanyo.

Mtafiti: Jina la Mtafiti linatakiwa kuwekwa kwa usahihi na kueleweka kwa majina yake yote kama yanavyojulikana na kuonekana kwenye vyeti na vitambulisho vyake.

Jinsia: Kwa wanyama wote wenye uti wa mgongo jinsia inatakiwa kurekodiwa. Pia mda mwingine alama zinaweza kutumika.

Vipimo: Vipimo maalumu vya ndege, wanyama, au viumbe vya baharini vinatakiwa kurekodiwa ipasavyo. Wasomaji wanashauriwa kufwata miongozo kama inafaa.

Namba ya mikusanyo: Kila kibandiko cha maelezo ya mkusanyo kinatakiwa kuwa na namba ya utambusho inayohusiana na maelezo ya utafiti ya mikusanyo hiyo.

Namba ya Katalogi: Wakati vielelezo vinaorodheshwa ni lazima vipewe katalogi namba kwenye vibandiko vya maelezo.

Utambulisho: Mapema wakati vielelezo vya mkusanyo vimetambuliwa , jina la kisayansi linatakiwa liwekwe pia kwenye kibandiko cha maelezo.

Ni vyema kama mikusanyo mingine imeambukizwa athari hii hutatuliwa kwa mikusanyo hiyo kutolewa na kuwekwa nje ili kuepuka kuzuia nafasi kwa mikusanyiko mingine. Dawa ambazo hutumika kuua wadudu huifadhiwa sehemu kavu kwenye unyevunyevu wa chini ya 55%. Kwa vielelezo ( Mikusanyo )vingine ambavyo dawa ya kupuliza haiwezekani kutumika, tumia kigodoro au kitambaa kikavu ambacho kililowekwa kwenye dawa.