Maonyesho ya Baolojia

MAONYESHO YA BIOLOJIA

Maonyesho ya Biolojia yanaonyesha jinsi viumbe hai vya Tanzania kupitia maonyesho ya safu ya Spishi wanaoishi katika mwingiliano wa mazingira na uhifadhi wa mazingira. Mazingira ya Majini na nchi kavu huwakilishwa vizuri na viumbe tofauti wa baharini na wa maji safi, savanna na misitu. Miongoni mwa maonyesho ya kuvutia ni ya "Nguva" ambaye hujibu swali la je mnyama huyu ni mamalia au "mermaid" na kudhaniwa kuwa ni samaki wa kihistoria "Coelacanth" alionekana miaka milioni 65 iliyopita na kuonekana tena Tanzania mwaka 2003. Kwa hiyo ukumbi wa Biolojia unachangia juhudi za Makumbusho kwa kuwatahadharisha umma majukumu muhimu kuhusu kuchezea viumbe hai ili kuendeleza maisha yao, mgogoro wa kiikolojia tunaokumbana nao unatusaidia kujua njia za kuhifadhi aina za spishi.