Akiolojia

AKIOLOJIA

Mikusanyo ya akiolojia ina jukumu muhimu katika kuendeleza elimu ya kisayansi na kushughulikia masuala yanayohusiana na maisha ya jamii za kale. Mikusanyo ya akiolojia iliyohifanyiwa katika Makumbusho ya Taifa itakupeleka katika ulimwenguwa kale kwa kuunganisha nyakati za kale na zasasa kwa kukuelezea ni jinsi gani binadamu katika wakati ule na maeneo tofauti aliweza kutumia uwezo/ujuzi aliokuwa nao kuhakikisha anaishi kwa kutumia vitu ambavyo vilipatikana katika mazingira ya nayowazunguka. Haya yanajihidhirisha kwa kupitia vionyeshwa vya akiolojia vinavyopatikana katika ukumbi wa maonyesho zikiwemo zama za mawe za miaka takribani 1.8 -1.5 milioni) mpaka zama za chuma takribani miaka 3,000 na kuendelea.

Makumbusho ya Taifa inahifadhi malikale mbalimbali za akiologia zinazopatikana katika maeneo mbambali ya kihistoria nchini. Malikale hizo ni pamoja na zana za mawe, zana za chuma, shanga, vyungu/vigae vya vyungu na kadhalika. Malikale hizo zimepangwa kutokana na mikoa na maeneo ambayo malikale hizo zilipatikana. Malikale zinazopatikana katika maeneo ya kihistoria hutofautiana kutoka eneo moja na jingine, kwa maana hiyo kuna maeneo ambayo nitajiri kwa kuwa na zama za mawe za mwanzo kama olduvai, Isimila, mtera, Natron, Mbeya, Eyasi. Maeneo kama Garusi (Eyasi iii), Senkenke, Lindi, Haubi yamekuwa na masalia mengi ya zama za mawe za kati wakati maeneo ya Eyasi, Ngorongoro (Eyasi iii), Sandawe /Apis, Kondoa, Kisese, Singida, Kiomboi-64, mbeya imetoa vielelezo vingi vya zama za mwisho za mawe. Hata hivyo kuna maeneo ya kihistoria ambayo ya meonyesha utajiri mkubwa wa malikale za vyungu pamoja na vitu vingine kama shanga na kadhalika maeneo hayo ni kama Kilwa, Ivuna, coastal, Mafia, DSM, Uvinza, Tanga na morogoro.

Lengo kuu la makusanyo yetu ya Akiolojia ni kuleta uelewa wa maisha ya jamii za kale kwa shule, walimu, watafiti, familia na vikundi mbalimbali vinavyotembela Makumbusho. Tumia mikusanyo yetu ya akiologia katika Makumbusho ya Taifa iliyo zaidi ya laki moja katika tafiti za kisayansi na program mbalimbali za kielimu na upate uelewa na uzoefu utakaokusaidia kupambanua mambo mbalimbali kuhusu jamii za kale na maisha yetu ya kila siku.