Mwakilishi wa Chansela wa Ujerumani atembelea Makumbusho ya Taifa

Imewekwa: 26th February, 2020

Mwakilishi wa Chansela wa Ujerumani anayeshughulikia Afrika, Bw Guenter Nooke ametembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kufurahisha na vionesho vilivyoko katika Makumbusho hiyo.

Bw. Nooke alikuwa ameongozana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi Regine Hess, na Dkt Rainer Hoening, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Batteri ya Ujerumanio.

Makumbusho ya Taifa walikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho, Dkt Noel Lwoga, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw. Achiles Bufure pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Makumbusho, Dkt Amandus Kweka.

Mwakilishi wa Chansela wa Ujerumani anayeshughulikia Afrika ametembelea ukumbi wa Chimbuko la Mwanadamu, Ukumbi wa Historia, pamoja na Onesho la Mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Ukombozi wa Afrika ambalo limepangwa katika ukumbi wa muda.

Akizungumza baada ya kutembelea kumbi hizo Bw Nooke amesema maonesho ni mazuri na kwamba ameyafurahia.